SWALI LA WIKI (JUMA 60)

SWALI: Nimekuwa nikisikia sana katika mazungumzi ya watu, wakisema neno “Istikhaara”, naomba kujua maana na makusudio ya neno hilo katika mtazamo wa dini yetu tukufu.

JIBU: Kwanza yataka ufahamu ya kwamba hiyo Istikhaara ni katika jumla ya matendo aliyo kuwa akiyaandama sana (akidumu kuyafanya) Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie. Hiyo Istikhaara ni jina linalo elezea rakaa mbili za Sunna anazo ziswali mja kisha zikafuatiwa na dua aliyo kuwa akiiomba Bwana Mtume. Mtume alikuwa akiswali rakaa mbili hizo, kila lilipo mtokea jambo au kila akijikuta mbele ya jambo ambalo hajui lina kheri au shari. Akisha swali, ikiwa jambo hilo lina kheri naye, hupata wepesi wa kulitenda au kulifikia na ikiwa lina shari, basi Allah humtilia uzito ndani yake. Na hapo ndipo Istikhaara kwa namna hiyo tuliyo itaja, ikawa ni Sunna yenye kufuatwa kutoka kwa Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie. Kunasuniwa kwa mtu anaye taka kufanya jambo, kama kuoa, kusafiri, kufanya kazi mahala na mambo kama hayo, kuswali swala ya Istikhaara na kuhitimisha na dua ambayo Mtume wa Allah alikuwa akiomba kupitia hiyo. Ikiwa jambo hilo lina kheri naye, basi Allah atakikunjua kifua chake na kumuwezesha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *