SWALI LA WIKI (JUMA 59)

SWALI: Katika zama zetu hizi za leo, tunaona watu wakiswali swala za Eid viwanjani au hata barabarani mbele ya msikiti. Naomba kujua sharia inasemaje kuhusiana na jambo hili?

JIBU: Ilivyo Sunna ya Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-ni kuswaliwa swala za Eid kwenye muswala (viwanjani vya wazi) na Mtume alikuwa akiziswali swala mbili hizo nje ya msikiti. Lakini pia imepokewa ya kwamba alipata kuswali swala ya Eid ndani ya msikiti, kwa sababu ya mvua.

Na Sunna hiyo iliendelezwa pia na makhalifa viongozi wa Bwana Mtume-Allah awawiye radhi. Na hali kadhalika imethibiti pia Sunna hiyo katika madhehebu ya Imamu Abu Hanifa na Imamu Ahmad bin Hambal-Allah awarehemu. Na Imamu Maalik-Allah amrehemu-anaona kwamba swala ya Eid ni Sunna (manduubu) kuswaliwa nje ya msikiti na ni karaha kuiswali msikitini pasina udhuru.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *