SUNNA ZILIZO(ZINAZOFUATIA) BAADA YA KUMALIZIKA SWALA

Hizi ni aina ya suna za swala ambazo huletea baada ya swala kumalizika. Hizi zinakusanya:-

1.  Kuleta Istighfaari, dhikri na dua.

Imepokelewa kwamba Mtume Rehama na Amani zimshukie alikuwa anapomaliza swala yake huleta Istingfaari mara tatu na kisha akasema.

ALLAHUMMA ANTASSALAAM, WA MINKASSALAAM, TABAARAKTA YAA DHALJALAAL WAL-IKRAAM

Muslim

 Si vibaya kunyanyua sauti kwa Imamu wakati wa kuleta Istighfaari, dhikri na dua, kwa lengo la kuwafundisha maamuma wake.

Wakishajua na kuzoea hasi walete dhikri hizo kwa sauti ya chini, isiyo ya kusikika kiasi cha kuwa ni kishawishi kwa watu wengine wanaoswali.

 Imepokelewa kutoka kwa Ibn Abbaas Allah awawiye radhi kwamba kunyanyua sauti kwa dhikri wakati watu wanapomaliza swala ya fardhi, kulikuwepo zama za Mtume – Rehema na Amani zimshukie.

Bukhaariy na Muslim.

 Imepokelewa kutoka kwa Ka’ab Ibn Ujirah – Allah amuwiye radhi kwamba Mtume Rehema na Amani zimshukie amesema

“Viandamizi, harejei patupu msemaji wake baada ya kila swala ya faradhi (Viandamizi hivyo ni) Tasbih (Sub-haanallaah) thelathini na tatu, Tahmiydah (Al-hamdulillaah) thelathini na tatu, na Takbiyrah (Allaahu Akbar) thelathini na tatu” Muslim

 Imepokelewa kutoka kwa Muaadh Ibn Jabal – Allah amuwiye radhi – kwamba Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukie alimshika mkono wake na kusema: “Ewe Muaadh, Wallah hakika mimi ninakupenda, akasema: “Ninakuusia ewe Muaadh, usiache usiache baada ya kila swala kusema:

ALLAHUMMA A’INNI ALAA DHIKRIKA WA SHUKRIKA WAHUSNI IBAADATIKA

Abuu Daawoud

Zipo dua na adhkaari nyingi sana za baada ya swala zilizopokewa kutoka kwa Bwana Mtume, unaweza kurejea vitabu vya hadithi na Adhkaari ikiwa unapenda kuzijua.

 

2.   Kugura kwa ajili ya swala ya suna kutoka mahala paliposwaliwa swala ya fardhi.

Ni suna iliyothibiti kutoka kwa Bwana Mtume, mtu kugura (kuhama) mahala aliposwalia swala ya fardhi kwa ajili ya kuswali  swala ya suna baada ya swala mahala pengine Falsafa ya suna hii ni kwamba mahala anaposujudu mja patamshuhudia mbele ya Allah, kuitekeleza suna hii hakutamaanisha kingine zaidi ya kukithiri kwa sehemu zitakazomshuhudia (zitakazomtolea ushahidi).

Lakini ni bora zaidi kama hakuna kipingamizi (dharura) kwenda kuswali swala ya suna  nyumbani kwake mtu baada ya kuiswali swala ya faradhi msikitini pamoja na jamaa. Hayo ndiyo maelekezo na mafundisho kutoka kwa Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie:

“Enyi watu, swalini majumbani mwenu, kwani bora ya swala ni mtu  kuswali nyumbani kweke ila swala ya fardhi” Bukhaariy na Muslim.

SUNNA ZILIZO(ZINAZOFUATIA) BAADA YA KUMALIZIKA SWALA

Hizi ni aina ya suna za swala ambazo huletea baada ya swala kumalizika. Hizi zinakusanya:-

1.  Kuleta Istighfaari, dhikri na dua.

Imepokelewa kwamba Mtume Rehama na Amani zimshukie alikuwa anapomaliza swala yake huleta Istingfaari mara tatu na kisha akasema.

ALLAHUMMA ANTASSALAAM, WA MINKASSALAAM, TABAARAKTA YAA DHALJALAAL WAL-IKRAAM

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *