Kutoa salamu ni ule ugeukaji wa kutumia shingo tu wa
mwenye kuswali kuliani kwake il-hali akisema
…………ASSALAAMU ALAYKUM WARAHMATULLAH
Nguzo hii ni natija ya kauli ya Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie
“ Ufunguo wa swala ni Twahara na Ihramu yake ni Takbiyra na ufunguzi wake ni Kutoa salamu”. Turmidhiy, Abuu Daawoud na wengineo.
Uchache wa salamu ni mtu kusema mara moja:
……………………………………… ASSALAAMU ALAYKUM
Ama ukamilifu wake ni kusema.
………………………………………. ASSALAAMU ALAYKUM WARAHMATULLAH
Mara mbili, mara ya kwanza kuliani na ya pili kushotoni.
Imepokelewa hadithi kutoka kwa Sa’ad – Allah amuwiye radhi – amesema :
Nilikuwa nikimuona Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukie – akitoa salamu kuliani kwake na kushotoni kwake mpaka ninaona weupe wa kitefute (shavu) chake” Muslim.