RUKUU

Nini rukuu.

Katika sheria, rukuu ni kuinama mwenye kuswali kiasi cha vitanga vyake kugusa magoti yake. Huu ndio uchache wa rukuu. Ama ukamilifu wake ni kuinama kiasic ha mgongo kulingana sawa na kufanya mfano wa pembe mraba (90o).

Rukuu  ndani ya Qur-ani.

Rukuu ndani ya Qur-ani inatajwa katika kauli tukufu ya Allah.

“ENYI MLIDAMINI RUKUUNI NA SUJUDUNI NA MUABUDUNI MOLA WENU NA FANYENI MEMA ILI MPATE KUFAULU (22:77).

Rukuu katika kivuli cha Sunnah:

Rukuu inatajwa katika kauli ya Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukie – aliposema kumfundisha mtu swala:

“….Kisha rukuu  mpaka utulizane ukiwa umerukuu……”  Bukhaariy na Muslim.

Sharti za rukuu.

Ili rukuu ya mwenye kuswali isihi kisheria ni lazima ajilazimishe kufuata yafuatayo

i)        Ainame kama tulivyoeleza katika kuainisha rukuu, yaani ainame mpaka vitanga viguse magoti.

Imepokelewa  na swahaba Abu Humayd – Allah amuwiye radhi – alipokuwa akitaja namna alivyokuwa akiswali Mtume wa Allah- Rehema na Amani zimshukie:

” …. Na anaporukuu huimanikinisha (huiweka) mikono yake magotini mwake……” Bukhaariy.

ii)       Asikusudie katika kurukuu kwake kitu kingine zaidi ya rukuu (kisichokuwa rukuu).

           Mathalan, iwapo mtu atainama kwa kuchelea kitu Fulani, akaendelea kuinama kwa kujaalia kuwa hiyo ndiyo rukuu,  rukuu hiyo haitoshi kwa hali hii kwa sababu haikukusudiwa kuwa ndio rukuu, bali ilikusudiwa kitu kingine.

           Katika mazingira kama haya itamuwajibikia asimame na alingane sawa, kisha ndipo arukuu kwa kuikusudia rukuu.

 

Atulizane katika rukuu kwa kadri ya Tasbihy moja kwa uchache. Hili linatokana na kauli ya Mtume iliyotangulia:

 “……Mpaka  utulizane ukiwa umerukuu….” Pia imepokewa kutoka kwa Mtume – Rehema na Amani zimshukie kwamba amesema

“Mwizi  muovu kuliko wote ni yule anayeiba ndani ya swala yake” (Maswahaba) wakauliza: Ewe Mtume wa Allah, mtu anawezaje kuiba katika swala yake? Akawajibu

“Hazitimizi rukuu zake (hiyo swala) wala sijida zake” Ahmad/Twabaraaniy.

NGUZO ZA SWALA 5.RUKUU

Nini rukuu.

Katika sheria, rukuu ni kuinama mwenye kuswali kiasi cha vitanga vyake kugusa magoti yake. Huu ndio uchache wa rukuu. Ama ukamilifu wake ni kuinama kiasic ha mgongo kulingana sawa na kufanya mfano wa pembe mraba (90o).

Rukuu  ndani ya Qur-ani.

Rukuu ndani ya Qur-ani inatajwa katika kauli tukufu ya Allah.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *