Kutungamanisha nguzo za swala ni kuziratibisha kwa utaratibu wake kama zilivyo moja baada ya nyingine kila moja ikachukua nafasi yake bila ya kuitangulia nyingine.
Kwa mantiki hii, mwenye kuswali analazimika kuianza swala yake kwa nia, halafu Takbiyra ya kuhirimia, kisha, asome Suratil-Faatiha, halafu arukuu, aitadili, asujudu……..na kuendelea kama hivi Angalia ikiwa mtu ataihamisha nguzo kwa makusudi kuitoa mahala pake ilipowekwa na sheria na kuipeleka mahala si pake, swala yake nzima itabatilika, haikubaliwi.
Ama akitenda hivyo bila ya kukusudia, basi swala yake itakuwa imebatilika kuanzia katika ile nguzo aliyoitenda mahala si pake na itamuwajibikia kuirudia swala yake tokea pale alipokosea tu.
Kwa mantiki, iwapo mtu ataendela na swala yake baada ya kuwa ameshabadili utaratibu wa nguzo mpaka akafikia mahala alipopabadilisha katika rakaa iliyotangulia.
Mathalann rukuu mpaka rukuu nyingine ya rakaa nyingine, nguzo shaihi ya rakaa hii ya sasa itakaa mahala pa nguzo fasidi ya ile rakaa iliyotangulia.
Kwa hivyo basi, itamuwajibikia azidishe rakaa moja, katika swala yake ili kuifidia ile rakaa iliyofisidika kwa kufisidika utaratibu wa nguzo.
(Allah ndiye Mjuzi mno wa lililo la sawa.)
Hizi ndizo nguzo za swala ambazo swala haisihi ila kwa kuzileta zote, tena kwa utaratibu huu tulioubainisha.
Ni wajibu kwa mwenye kuvaana na ibada hii awaye yeyote, mwanamume wau mwanamke aihifahdi ibada hii kwa kuiteleza kwa ikhlasi, ufanisi na unyenyekevu.