MAMBO YANAYOSABABISHA JANABA

Janaba husababishwa na mambo mawili yafuatayo :

i. Mwanamume/Mwanamke kutokwa na manii kwa sababu yeyote miongoni mwa sababu zake kama vile kujiotelea usingizini yaani mtu kuota usingizini kuwa anafanya tendo la ndoa.

Au yakatoka kwa kuchezeana na kushikana baina ya mwanamume na mwanamke.

Au yakatoka na athari ya kutazama/kufikiri kulikouathiri moyo.

Sasa ni vema tukajua manii ni nini ? Manii kwa upande wa mwanamume ni maji meupe, mazito yachupayo ambayo hutoka wakati anapofikia kilele cha matamanio.

Ama upande wa mwanamke ni maji ya manjano na ni mepesi. Katika jumla ya dalili za kuthibitisha kuwa utokaji wa manii huwajibisha josho ni hadithi zifuatazo :

 o     Imepokelewa na Ummu Salamah – Allah amuwie radhi – amesema :

Ummu Sulaym alikuja kwa Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukie akasema : Ewe Mtume wa Allah, bila shaka Allah haoni haya kusema haki, je, inampasa mwanamke kuoga atakapojiotelea ? Mtume akajibu :

Naam, atakapoyaona maji (manii)” Bukhariy na Muslim.

o  Imepokelewa na Mama Aysha –Allah amuwie radhi – kwamba Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukie – aliulizwa kuhusiana na mwanamume anayekuta ubichibichi/umajimaji (athari ya manii) na wala hakumbuki kujiotelea.

Mtume akajibu “(Atapaswa) kukoga

Na aliulizwa pia juu ya mwanamume mwenye kuona kajiotelea lakini hakukuta ubichibichi. Akasema “Haimpasi kukoga”.

Ummu Sulaym akasema :

Mwanamke (pia) huona hivyo (hujiotelea), je, inampasa kukoga ? (Mtume) akajibu :

“Naam, wanawake ni ndugu baba mmoja, mama mmoja na wanamume” Abu Dawoud.

Muradi wa kauli ya Mtume ni kuwa wao (wanamume na wanawake) ni sawa sawa katika nyenendo na tabia za kimaumbile.

 ii Jimai – Yaani kujamiiana hata kama manii hayakutoka.

Mwanamume akiingiza sehemu tu ya dhakari yake katika tupu ya mwanamke, basi imewapasa wawili hao; mwanamume na mwanamke huyo kukoga josho la kisheria bila ya kuangalia wametokwa na manii au la.

Kinachozingatiwa hapa ni muingiliano na mvaano wa tupu mbili hizo, ya mwanamume na mwanamke na si utokaji wa manii.

Imepokelewa na Abu Hurayrah –Allah amuwie radhi- kutoka kwa Mtume –Rehema na Amani zimshukie – amesema :

” Mwanamume akikaa baina ya mapaja na miundi yake (mwanamke), halafu akamuendesha mbio, hakika limekwishapasa josho” Bukhariy na Muslim.

Na katika upokezi wa Imaam Muslim kuna ziada : “Hata kama hakutokwa na manii”.

Na katika hadithi nyingine iliyopokelewa na Mama Aysha – Allah amuwie radhi –

“Na khitani ikiigusa khitani (dhakari ikaigusa tupu ya mwanamke) hakika limepasa josho (kwa wote wawili)” Muslim.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *