MAMBO YALIYO HARAMU KWA MWENYE JANABA

Mtu akipatwa na janaba kwa maana ya janaba kama tulivyoeleza katika maelezo yetu ya awali yanamuharimikia kwa mujibu wa sheria mambo yafuatayo:-

1.      Kuswali swala ya fardhi au ya sunnah. Hili ni kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 “ENYI MLIOAMINI! MSIKARIBIE SWALA, HALI MMELEWA MPAKA MYAJUE MNAYOSEMA WALA HALI MNA JANABA ISIPOKUWA MMO SAFARINI (mnapita njia) MPAKA MKOGE…” [4:43]

Muradi na makusudio ya neno SWALA katika aya hii ni MAHALA PA KUSWALIA (msikiti) kwa sababu kupita njia hakupatikani ndani ya swala.

Ikiwa mwenye janaba anakatazwa kupita msikitini, basi kukatazwa kuswali ni aula zaidi.

Amepokea Imam Muslim kutoka kwa Ibn Umar- Allah awawiye radhi- amesema : Hakika nimemsikia Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukie- akisema

“Haikubaliwi swala bila ya twahara”.

Twahara iliyotajwa katika hadithi ni pamoja na twahara ya hadathi ndogo na janaba (hadathi kubwa).

Hadathi hii inafahamisha uharamu wa kuswali kwa mwenye hadathi zote hizo; hadathi ndogo na hadathi kubwa(janaba).

 

2.      Kukaa msikitini. Ama kupita njia tu bila ya kukaa si haramu. Haya yanafahamika kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu :

 “…WALA HALI MNA JANABA, ISIPOKUWA MMO SAFARANI(mnapita njia)…”.

 Yaani msiikurubie swala wala mahala pa kuswali (msikiti) mtakapokuwa mna janaba bila kukurubia kwa nia ya kupita njia, huku hakukukatazwa.

Naye Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Msikiti si halali kwa mwenye hedhi wala mwenye janaba”. Abu Daawoud

 

3.      Kutufu Al-Kaaba , twawafu ya nguzo/fardhi au ya sunna.

Hii ni kwa sababu twawafu iko katika daraja ya swala, kwa hiyo nayo imeshurutizwa twahara kama ilivyo kwa swala.

Haya ni kwa mujibu wa kauli ya Bwana Mtume –Rehema na Amani zimshukie- aliposema:

“Kutufu al-Kaaba ni swala, isipokuwa kwamba Allah amekuhalalishieni kuzungumza ndani yake (twawafu), basi atakayazungumza na asizungumze ila la kheri”. Al-Hakim

 

4.      Kusoma Qur-ani. Amesema Nabii Muhammad Rehema na Amani zimshukie:

“Asisome mwenye hedhi wala mwenye janaba chochote katika Qur-ani”. Tirmidhiy

ANGALIA: Inajuzu kwa mwenye janaba kuisoma Qura-ani moyoni bila ya kuitamka kwa ulimi, kama ambavyo inavyomjuzia kuutazama Msahafu bila kuushika.

Kadhalika inamjuzia kusoma dhikri/nyiradi za Qur-ani kwa kukusudia ile dhikri na sio Qur-ani yenyewe.

Dhikri ya Qur-ani ni kama vile mtu kusema:


(RABBANAA AATINAA FID-DUN-YAA HASANATAN WAFIL AAKHIRATI HASANATAN WAQINAA ADHAABAN-NAAR)[2:201] kwa kuikusdua aya hii kama dua.

Na kama vile kusoma anapokipanda kipando (chombo cha usafiri)

(“SUB-HANNAL-LADHIY SAKHARA LANNA HAADHA WA MAA KUNNAA LAHU MUQRINIYN”) [43:13] kwa kuisudia hii dua na sio dhati ya Qur-ani yenyewe. Allah ndiye mjuzi mno.

 

5.  Kuugusa au kuubeba /kuuchukua msahafu au karatasi/kataa la msahafu au ngozi/jalada lake au kuuchukua msahafu ukiwa ndani ya mfuko au sanduku. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“HAPANA AKIGUSAYE ILA WALE WALIOTAKASWA” [56:79]

Bwana Mtume –Rehema na Amani zimshukie- anatufasiria aya hiyo kwa kusema :

“Asiiguse Qur-ani ila aliye twahara “. Daaruqutuniy na Maalik.

 

ANGALIA: Inajuzu kwa mwenye janaba kuubeba msahafu ukiwa pamoja na mizigo au ndani ya nguo sandukuni na wala hakuukusudia kuubeba ule msahafu bali mizigo/nguo.

Kadhalika inamjuzia kuvichukua vitabu vya tafsiri ya Qur-ani iwapo ile tafsiri ni nyingi kuliko Qur-ani. Allah ndiye mjuzi mno wa lililo la sawa na haki.

 

MAMBO YALIYO HARAMU KWA MWENYE JANABA

Mtu akipatwa na janaba kwa maana ya janaba kama tulivyoeleza katika maelezo yetu ya awali yanamuharimikia kwa mujibu wa sheria mambo yafuatayo:-

1.      Kuswali swala ya fardhi au ya sunnah. Hili ni kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 “ENYI MLIOAMINI! MSIKARIBIE SWALA, HALI MMELEWA MPAKA MYAJUE MNAYOSEMA WALA HALI MNA JANABA ISIPOKUWA MMO SAFARINI (mnapita njia) MPAKA MKOGE…” [4:43]

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *