Fiq-hi ni neno la kiarabu lenye maana mbili.
Maana ya kwanza ni ya kilugha na ya pili ni ya kisheria.
Katika lugha ya kiarabu neno “fiq-hi” maana yake ni kufahamu na kujua.
Fiq-hi kwa mtazamo wa sheria ni fani ya elimu inyoshughulikia na kusimamia utekelezaji wa sheria, kanuni na na taratibu za Uislamu katika maisha ya kila siku.
Kwa ujumla fiq-hi ni sheria zinazoyatawala maisha ya Muislamu katika nyanja zote za maisha, kuanzia elimu, ibada, uchumi, ulinzi na usalama, ndoa, mirathi na kadhalika.