KUSUJUDU MARA MBILI KATIKA SWALA

Nguzo ya saba ya swala ni kusujudu. Na maana ya sijida ni kugusa paji la uso la mswaliji mahala anapo sujudu.


Dalili ya sijida: Sijida kama nguzo ya swala ni agizo na amri ya Allah itokanayo na kauli yake tukufu:

“ENYI MLIO AMINI! RUKUUNI NA SUJUDUNI NA MUABUDUNI MOLA WENU NA FANYENI MEMA, ILI MPATE KUFAULU”.2


Na kauli yake Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-alipo mwambia yule mtu aliye kosea katika swala yake:

“…Kisha sujudu mpaka utulizane hali ya kusujudu. Halafu inuka utulizane hali ya kukaa, halafu sujudu (tena) mpaka utulizane hali ya kusujudu…”.


Sharti za sijida:


Ili sijida iswihi kisheria, kumeshurutizwa kuchunga mambo yafuatayo:


a)  Paji la uso liwe wazi wakati wa kugusana na ardhi.


b)  Kusujudu kuwe ni kwa viungo saba alivyo vitaja Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-kupitia kauli yake:

“Nimeamrishwa kusujudu kwa (kutumia) mifupa (viungo) saba; Juu ya paji la uso – na akaashiria kwa mkono wake pua yake – na mikono na miguu na ncha za (vidole vya) miguu”.3
Tanbihi: Si wajibu kuacha wazi chochote katika viungo saba hivi vilivyo tajwa ila paji la uso tu.


c)  Sehemu yake ya chini (kiuno) iinuke zaidi kuliko ile ya juu (mabega) kiasi kimkinikacho. Kufanya hivyo ni kufuata kitendo cha Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie.


d)   Hasisujudu juu ya nguo iliyo ambatana naye inayo tukutika kwa mtukutiko wake, mithili ya kilemba au kashida yake.


e)   Hasikusudie kitu kingine chochote zaidi ya sijida, mithili ya kuporomoka kwa ajili ya hofu.


f)   Kukandamiza kidogo paji lake katika ardhi kwa sura ambayo kama ingekuwepo hapo anapo sujudu pamba au kitu mithili ya pamba, ingebonyea na athari ya sijida kudhihiri hapo.


g)  Kutulizana katika sijida kwa kadiri ya kuleta Tasbihi moja.
Na ukamilifu wa sijida ni mswaliji kuleta Takbira ya kuporomokea sijida na kuweka ardhini magoti yake yakifuatiwa na mikono.

Halafu paji na kumalizia na pua yake na aiweke mikono yake welekeya (mkabala) wa mabega yake na avitandike vidole vyake kwa kuvikusanya vikiwa vimeelekezwa Qiblah.

Na aliepushe tumbo lake kugusana na mapaja yake, na dhiraa zake zisigusane na ardhi wala mbavu zake. Na aseme mara tatu: SUB-HAANA RABBIYAL-A’ALAA.

Imepokelewa kutokana na hadithi ya Abu Hurayra-Allah amuwiye radhi-katika kuielezea swala ya Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie:

“…Kisha husema: ALLAAHU AKBAR, wakati aporomokapo hali ya kusujudu…”.4


Na imepokelewa kutoka kwa Abdillah Ibn Maalik Ibn Buhaynah-Allah amuwiye radhi-kwamba

“Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-alikuwa anaposwali, huweka mwanya baina ya mikono yake mpaka unaonekana weupe wa kwapa zake”.5


Imepokewa kutoka kwa Al-Baraai-Allah amuwiye radhi-amesema: Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-amesema:

“Unapo sujudu, basi weka vitanga vyako (ardhini) na vinyanyue viko (mirfaq) vya mikono yako”.6
Na imepokewa katika kutaja wasifu wa swala ya Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie:

 “…na anapo sujudu, husema katika sijida yake: SUB-HAANA RABBIYAL-A’ALAA, mara tatu…”.7
Tanbihi: Mwanamke huhitilafiana na mwanaume katika baadhi ya vipengele tulivyo vitaja. Yeye ataukusanya pamoja mwili wake wakati wa kusujudu.

Imepokelewa kwamba Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-aliwapitia wanawake wawili hali ya kuwa wanaswali, akawaambia:

Mnapo sujudu (kuelekea ardhini), basi zikusanyeni baadhi ya nyama, kwani mwanamke siyo kama mwanaume katika hilo”.8

KUSUJUDU MARA MBILI KATIKA SWALA

Nguzo ya saba ya swala ni kusujudu. Na maana ya sijida ni kugusa paji la uso la mswaliji mahala anapo sujudu.

Dalili ya sijida: Sijida kama nguzo ya swala ni agizo na amri ya Allah itokanayo na kauli yake tukufu:

“ENYI MLIO AMINI! RUKUUNI NA SUJUDUNI NA MUABUDUNI MOLA WENU NA FANYENI MEMA, ILI MPATE KUFAULU”.2

Na kauli yake Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-alipo mwambia yule mtu aliye kosea katika swala yake:“…Kisha sujudu mpaka utulizane hali ya kusujudu. Halafu inuka utulizane hali ya kukaa, halafu sujudu (tena) mpaka utulizane hali ya kusujudu…”.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published.