KUSUBIRI NJE YA MLANGO WAKATI BWANA HARUSI ANAPOINGIA NDANI ILI KUJUA KAMA BI. HARUSI NI BIKRA

Athari ya ada hii mbaya bado imesalia katika ndoa za baadhi ya jamii zetu. Bwana harusi anapofunga ndoa na kisha kumchukua mkewe nyumbani kusindikizwa na jamaa hasa wanawake wa pande zote mbili; upande wake na ule wa mkewe.

 

Chumba cha bwana harusi hupambwa vizuri na kitanda kutandikwa shuka maalum mpya, hili si baya. Baya na la aibu lisilokubalika ni baada ya Bwana na Bi. Harusi kuingia chumbani baadhi ya akina mama husubiri nje mlangoni wakati mtu na mkewe wanapofanya tendo la ndoa. Hawa husikiliza kwa makini iwapo bi harusi atalia kutokana na maumivu ya kuvunjwa bikira yake.

 

Wakishalisikia walitakalo, hapo ndipo maharusi hugongewa mlango, mlango ukishaunguliwa akina mama hawa hujitoma ndani kwa nderemo na vifijo, wakakichukua kitambaa kilicholowa na kuchafuliwa na damu wakatoka nacho nje huku wakishangilia na kukionyesha kwa watu wakisema: “Harusi imejibu.”

 

Ndugu zaguni, hii ni fedheha isiyo na nafasi hata kidogo katika maadili na mafundisho sahihi ya uislamu. Huku ni kumdhalilisha utu wa binadamu, kuvunja heshima na haki yake ya uwa faraghani. Qur-ani inatuambia: “NA HAKIKA TUMEWATUKUZA WANAADAMU….” (17:70).

 

Tendo la ndoa ni tendo tukufu sana, kwani ndilo ambalo Mwenyezi Mungu Mtukufu amelijaalia liwe ni sababu ya kuendeleza kizazi cha binadamu, binadamu muzaane kupitia tendo hilo. Tendo hili huhitaji faragha ya kutosha kumuaminisha kila mmoja kati ya mume na mke kwa wako peke yao tu na wa tatu wao ni yule aliywahalalishia wao tendo hilo yaani Mola wao, hapo ndipo hupatikana utulivu wa kulifanya tendo hili kwa makini, furaha na ukamilifu.

 

Huo ndio ubinadamu unaomtofautisha hayawani huyu binadamu na hayawani wengine katika tendo hili la kuzaana. Kwa hivyo hairuhusiwi kabisa kisheria kuingilia kati faragha hii, kufanya hivyo hakumaanishi kingine zaidi ya kudhulumu na kunyang’anya haki ya faragha ya watu wengine. Isitoshe kukionyesha kwa watu kitambaa chenye damu ni kumdhalilisha huyu mwanamke masikini, mwenye haki ya kujua kuwa mke ni bikira au thayibu (siyo bikira) ni mume tu na sio watu wengine.

 

Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie, anatumbia; “Huenda mwanamume akazungumza (kwa watu) kile kinachokuwa baina yake na mkewe au huenda mwanamke (pia) akazungumza kitendo kinachokuwa baina yake na mumewe, (kama yuko afanyae hivyo) basi msifanye hivyo, kwani huo ni mfano wa shetani mwanamume aliyekutana njiani na shetani mwenzake mwanamke, akamuingilia huku watu wakiangalia.”Twabaraaniy.

 

Sasa ikiwa mume/mke hana haki ya kuitoa nje siri ya unyumba wao, na Bwana Mtume akamfananisha mume/mke afanyaye hivyo na shetani. Vipi, wewe usiye mume/mke unaipata wapi ruhusa na na kibali hiki cha kukfichua na kuitoa nje siria hii ya mke na mume (bikira)? Je, hujioni kwamba wewe ni mbaya zaidi kuliko shetani ? Tuacheni ndugu zanguni, mambo haya hayakubaliani hata na akili tu ya kawaida, seuze dini/mfumo sahihi wa maisha! 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *