Inakupasa ufahamu kwamba kusoma Al-hamdu, ndio nguzo ya nne ya swala yeyote ile iwayo ya suna au ya fardhi na ni katika kila rakaa.
Nguzo hii inamuwajibikia Imamu, maamuma na hata mwenye kuswali pekee (Munfaridu). Nguzo hii haisamehewi ila kwa maamuma aliyemdiriki Imamu katika rukuu.
Huyu atanuia na kuhirimia, halafu aungane na Imamu katika rukuu na atahesabiwa kuwa ameipata rakaa hii ijapokuwa hakuisoma al-hamdu.
Suna na usomaji wa Al-hamdu.
1. Amesema Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie:
“Hana swala mtu asiyesoma Faatihatul-kitaab” (Al-hamdu)”. Bukaariy na Muslim
Tanbihi:
Bismillah ni miongoni mwa aya za Suuratil-faatihah. Haisihi suuratil–faatihah bila ya mwenye kuswali kusoma (Bismillahir_Rahmaanir-Rahiym).
Haya ni kwa mujibu wa riwaya iliyopokelewa na Ibn khuzaymah-kutoka kwa Ummu Salamah-Allah amuwiye radhi – kwamba Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie – aliihesabu (Bismillahri – Rahamaanir – Rahiym) kuwa ni aya katika Suuratil-Faatihah.
Sharti za kusihi Al-hamdu.
Mwenye kuswali, hana budi kuchunga sharti zifuatazo anapoisoma Suuratil-Faatiha:.
i) Msomaji ajisikizishe Suuratil-Faatihah iwapo hana matatizo ya kusikia.
ii) Akitungamanishe kisomo cha Suuratil-Faatihah, yaani azisome aya zake kwa utaratibu kama ilivyopokewa kutoka kwa Bwana Mtume na ilivyonakiliwa leo msahafuni. Aisome huku akichunga matokeo ya herufi na hukumu zote za usomaji.
iii) Katika usomaji wake, hasifanye kosa linaloweza kuharibu maana mathalan neno(An-amta) akalitamka (An-amtu) hapo maana itakuwa imeharibika.
Kwani badala ya maana kuwa “Umeneemesha wewe Allah” itakuwa “Nimeneemesha mimi”.
Lakini akifanya kosa lisilo na athari katika maana swala yeke haitabatilika bali itamuwajibikia ajifundishe matamshi sahihi.
Kosa hili ni kama vile kusoma“Al-Hamdu Lillahi Rabbul-Aalamin”
Badala ya “Al-Hamdu Lillahi Rabbil-Aalamin” Akaweka harakati ya dhummah katika neno “rabbu” badala ya harakah ya kasra “rabbi” ambayo ndiyo stahiki ya neno hilo hapo lilipo.
Makosa kama haya hayaharibu maana ijapokuwa yanabakia kuwa ni makosa ya kisarufi.
iv) Aisome kwa lugha ya Kiarabu, haisihi kuisoma kwa lugha nyingine kwa sababu hiyo haitakuwa Qur-ani bali tafsiri ya Qur-ani.
v) Aisome akiwa amesimama. Akienda rukuu huku anakamilisha kuisoma, usomaji wake huo utabatilika na itamuwajibikia kurudi katika kisimamo na kusoma tena.
Inakupasa ufahamu kwamba kusoma Al-hamdu, ndio nguzo ya nne ya swala yeyote ile iwayo ya suna au ya fardhi na ni katika kila rakaa.
Nguzo hii inamuwajibikia Imamu, maamuma na hata mwenye kuswali pekee (Munfaridu). Nguzo hii haisamehewi ila kwa maamuma aliyemdiriki Imamu katika rukuu.
Huyu atanuia na kuhirimia, halafu aungane na Imamu katika rukuu na atahesabiwa kuwa ameipata rakaa hii ijapokuwa hakuisoma al-hamdu.
Suna na usomaji wa Al-hamdu.
1. Amesema Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie:
“Hana swala mtu asiyesoma Faatihatul-kitaab” (Al-hamdu)”. Bukaariy na Muslim
Tanbihi:
Bismillah ni miongoni mwa aya za Suuratil-faatihah. Haisihi suuratil–faatihah bila ya mwenye kuswali kusoma (Bismillahir_Rahmaanir-Rahiym).
Haya ni kwa mujibu wa riwaya iliyopokelewa na Ibn khuzaymah-kutoka kwa Ummu Salamah-Allah amuwiye radhi – kwamba Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie – aliihesabu (Bismillahri – Rahamaanir – Rahiym) kuwa ni aya katika Suuratil-Faatihah.
Sharti za kusihi Al-hamdu.
Mwenye kuswali, hana budi kuchunga sharti zifuatazo anapoisoma Suuratil-Faatiha:.
i) Msomaji ajisikizishe Suuratil-Faatihah iwapo hana matatizo ya kusikia.
ii) Akitungamanishe kisomo cha Suuratil-Faatihah, yaani azisome aya zake kwa utaratibu kama ilivyopokewa kutoka kwa Bwana Mtume na ilivyonakiliwa leo msahafuni.
Aisome huku akichunga matokeo ya herufi na hukumu zote za usomaji.
iii) Katika usomaji wake, hasifanye kosa linaloweza kuharibu maana mathalan neno(An-amta) akalitamka (An-amtu) hapo maana itakuwa imeharibika. Kwani badala ya maana kuwa
“Umeneemesha wewe Allah” itakuwa “Nimeneemesha mimi”.
Lakini akifanya kosa lisilo na athari katika maana swala yeke haitabatilika bali itamuwajibikia ajifundishe matamshi sahihi. Kosa hili ni kama vile kusoma“Al-Hamdu Lillahi Rabbul-Aalamin”
Badala ya “Al-Hamdu Lillahi Rabbil-Aalamin” Akaweka harakati ya dhummah katika neno “rabbu” badala ya harakah ya kasra “rabbi” ambayo ndiyo stahiki ya neno hilo hapo lilipo. Makosa kama haya hayaharibu maana ijapokuwa yanabakia kuwa ni makosa ya kisarufi.