KUSIMAMA KWA MWENYE KUWEZA KATIKA SWALA YA FARADHI

Kuswali kwa kusimama katika swala ya fardhi ndiyo nguzo ya pili ya swala. Nguzo hii

inamuhusu mtu aliye mzima, anayeweza kusimama bila ya taabu. Haya ni kwa  mujibu wa kauli tukufu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya Qur-ani Tukufu.

“ANGALIENI SANA SWALA (Zote kuziswali, khasa jamaa) NA (khasa) ILE SWALA YA KATI NA KATI NA SIMAMENI KWA UNYENYEKEVU KATIKA KUMUABUDU ALLAH”(2:238).
     

    Mradi na mapendeleo ya kauli (NA SIMAMENI KWA UNYENYEKEVU) ni kisimamo cha ndani ya swala.

     Dalili ya nguzo hii katika sunna.

      Imepokelewa na Imraan Ibn Huswayn-Allah amuwiye radhi – amesema: Nilikuwa na maradhi ya Bawasiri, nikamuuliza Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie – juu ya swala (niswali vipi)? Akanijibu

     ” Swali kwa kusimama, ikiwa hauwezi (kusimama) swali kwa kukaa na kama hauwezi (kukaa) basi swali kwa kulalia ubavu”.  Bukhaariy

      Mtu atazingatiwa kuwa amesimama pale atakapokuwa  amenyooka wima, hakuinamia mbele au nyuma, kuliani na kushotoni.

     Akisimama kwa kupinda/kuinama japo kidogo bila ya udhuru kama uzee au maradhi swala yake itabatiklika, kwa sababu ya kukosekana nguzo ya kusimama ambayo ni sehemu inayounda swala.

      Mtu akiweza kuswali kwa kusimama katika baadhi ya swala na kushindwa katika baadhi nyingine, huyu atasimama pale awezapo kusimama na atakaa pale asipoweza.

      Ama kwa upande wa swala za sunnah, inajuzu mtu kuziswali akiwa amekaa hata  kama anaweza kusimama.

     Lakini atambue kuwa thawabu  anazozipata kwa kuswali akiwa amesimama ni nyingi zaidi kuliko zile atakazozipata kwa kuswali akiwa amekaa.

     Haya yanatokana na kauli ya  Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie: 

      “Atakayeswali kwa kusimama ndio bora, na atakayeswali kwa kukaa ana nusu ya ujira wa aliyesimama , na mwenye kuswali kwa kulala ana nusu ya ujira wa aliyekaa” Bukhaariy.

TANBIHI:

Atakayeshindwa kusimama katika swala ya fardhi na akaswali kama awezavyo kwa kuwa

“ALLAH HAIKALIFISHI NAFSI YOYOTE ILA YALIYO SAWA NA UWEZA WAKE………”(2:286)  atapata ujira  wake kamili sawa na yule aliyesimama.

Hivyo ndivyo inavyosema hadithi iliyopokelewa na Abu Muusa Al-ash-ariy-Allah amuwiye radhi – kwamba Mtume–Rehma na amani zimshukie – amesema .

”Mja atakapoumwa au kusafiri, Mwenyezi Mungu atamuandikia (thawabu) za aliyokuwa akiyatenda naye mzima mkazi (haumwi na hayuko safarini] “ Bukhaariy.  

 

KUSIMAMA KWA MWENYE KUWEZA KATIKA SWALA YA FARADHI

Kuswali kwa kusimama katika swala ya fardhi ndiyo nguzo ya pili ya swala. Nguzo hii

inamuhusu mtu aliye mzima, anayeweza kusimama bila ya taabu. Haya ni kwa  mujibu wa kauli tukufu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya Qur-ani Tukufu.
“ANGALIENI SANA SWALA (Zote kuziswali, khasa jamaa) NA (khasa) ILE SWALA YA KATI NA KATI NA SIMAMENI KWA UNYENYEKEVU KATIKA KUMUABUDU ALLAH”(2:238).

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *