Ndoa ni suala nyeti kabisa katika maisha ya mwanadamu. Unyeti wa suala hili la ndoa unajidhihirisha kutokana na umuhimu wa ndoa katika kuendeleza kizazi cha wanadamu ambalo hili ni tunda kuu la ndoa.
Kadhalika unyeti wa ndoa unatokana na haja tegemezi ya mwanamume kwa mwanamke na mwanamke kwa mwanamume.
Katika hali ya kawaida kimaumbile mwanadamu na mwanamke ni jozi (pair) tangamano, hii inamaanisha kwamba kila mmoja anamuhitajia mwenziwe ili kukamilika kimaumbile.
Ni kwa kuuzingatia unyeti huu ndipo sheria ikalitawala eneo zima la ndoa, kabla na baada ya ndoa.
Uislamu ukaweka na kupanga taratibu/kanuni na sheria ambazo muumini ni lazima azifuate katika utekelezaji wa suala zima la ndoa.
Sheria/taratibu hizi huanzia tangu katika ile hatua ya awali kabisa ya uchumba, ambayo hii hutufikisha katika posa, utoaji wa mahari, ndoa yenyewe ikiwa ni pamoja na sherehe/hafla zinazoambatana na ndoa na hatimaye kutia nanga katika maisha ya ndoa.
Maeneo yote haya tayari yameshaguswa na kuwekewa sheria na taratibu amazo zimefafanuliwa kiufasaha kabisa na Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie- kupitia kauli na matendo halisi.
Kwa mantiki hii muislamu hana nafasi ya kujiundia taratibu zake mwenyewe zinazopingana na sheria. Kufanya hivyo ni kosa, na mtendaji anastahili kubeba mzigo na dhamana ya kosa lake hilo. Tusome, tutafakari na tuzingatie:
“…………..NA NI NINI KIKO BAADA YA (kuacha) HAKI ISIPOKUWA UPOTEVU, BASI MNAGEUZWA WAPI ? (10:32)
Baada ya kuwekana sawa kwa utangulizi huo, hebu sasa tuanze kuizungumzia mada yetu. Pengine tunaweza kujiuliza kwa nini tumeigusa ndoa wakati mada yetu kuu ni Bi. Harusi?
Tumefanya hivyo kwa sababu hatuwezi kumpata na kuwa na Bi harusi bila kuwepo ndoa, Bi. Harusi ni zao la ndoa. Haya sasa tukiangalie kwa pamoja kipengele chetu cha kwanza.
(a) KUMTOA HADHARANI BI. HARUSI
Imezoeleka, imekuwa kawaida na mtindo katika jamii zetu kumtoa nje bi. Harusi baada ya ndoa kufungwa na hili hufanyika mbele ya kadamnasi ya wanamume na wanawake.
Ada hii imeendelea mpaka kufikia hatua ya kuonekana kuwa ina upungufu na haikukamilika ndoa ambayo imefungwa bila ya Bi. Harusi kutolewa nje na kuonyeshwa hadharani. Tunasema hivyo ndivyo tunavyofanya katika harusi zetu na tumezoea au kuzoeshwa hivyo.
Lakini je, hayo ndiyo maelekezo na mafundisho ya Uislamu au ni matashi na matamanio ya nafsi zetu? Tukubali au tukatae, huku ni kupingana na sheria na ni upotevu unaotokanan na kumfuata shetani – mlaaniwa – ambaye ni adui yetu mkubwa.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuasa na kutuamrisha;
“ENYI MLIOAMINI! INGIENI KATIKA HUKUMU ZA UISLAMU ZOTE, NA WALA MSIFUATE NYAYO ZA SHETANI, KWA HAKIKA YEYE KWENU NI ADUI DHAHIRI.” (2:208)
Kuendeleza mila na ada hii ni kumdhulumu Bwana harusi, ambaye ndiye mwenye haki na mkewe (Bi. Harusi). Sasa ikiwa yeye ndiye mwenye haki, sisi tunamuonyesha nani uzuri, kupendeza na mapambo ya mkewe?
Ni dhahiri kuwa katika siku hiyo muhimu kabisa katika maisha ya mwanadamu, Bi. Harusi hupambwa na akapambika na hali halikatazwi na sheria muda wa kuwa ni mapambo halali yanayokubalika kisheria. Sasa tunapo