KUMSALIA MTUME BAADA YA TASHAHADU YA MWISHO

Hii ndio nguzo ya kumi na moja ya swala. Nguzo hii yaani

kumswalia Bwana Mtume, huchukua nafasi mara tu bada ya kukamilka kwa tashahudi na kabla ya kutoa salamu. Hapo ndipo mahala pake nguzo hii.

 

Dalili ya swala  ya Mtume.

Kumswalia Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie – ndani ya swala ni katika kulitekeleza agizo na amri ya Allah isemayo

“HAKIKA ALLAH ANAMTEREMSHIA REHEMA MTUME (anaswalia) NA MALAIKA WAKE (wanamuombea dua) BASI, ENYI WAUMINI MSWALIENI (Mtume, muombeeni rehema) NA MUOMBEENI AMANI” (33:56).

Wanazuoni wamekongamana na kuwafikiana kwamba kumswalia Mtume si WAJIBU ila ndani ya swala tu. Uwajibu huu unatokana na riwaya nyingi sahihi ikiwemo hii iliyopokelewa kutoka kwa Ibn Masoud – Allah amuwiye radhi – katika (kueleza) swali aliloulizwa Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie – juu ya kuswaliwa kwake.

Tukuswalieje ndani ya swala? Akajibu, Semeni.

ALLAHUMMA SALLI ALAA MUHAMMAD WA ALAA AALI MUHAMMAD KAMAA SALLAYTA ALAA IBRAHIM WA AALI IBRAHIM WABAARIK ALAA MUHAMMAD WA ALAA AALI MUHAMMAD KAMAA BAARAKTA ALAA IBRAHIM WA ALAA AALI IBRAHIM FIL-AALAMINA INNAKA HAMIDUN MAJID  Bukhariy na Muslim

Riwaya hii ndio inayoanisha kwamba mahala pa wajibu pa kumswalia Bwana Mtume ni ndani ya swala.

Uchache wa matamko ya kumswalia Mtume ni  kusema:

……………ALAAHUMMA SALLI ALAA MUHAMMAD

Matamko kamili ni kamili ni kama hayo yaliyomo ndani ya hadithi tuliyoitaja. Katika baadhi ya riwaya kuna zaida au pungufu.

Sharti za swala ya Mtume.

Kumeshurutizwa katika kumswalia Mtume ndani ya Swala, kuchunga mambo yafuatayo:-

 (i)  Ajisikilizishe mwenyewe matamko yake, iwapo hana matatizo ya usikivu.

 (ii)Iwe ni kwa tamko la “ Muhammad” au Rassul” au “An-nabiy”. Lau mtu atamswalai kwa kusema mathalan “Alaa Ahmad”, haitamjuzia.

 (iii)  Iwe ni kwa Kiarabu.

Akishindwa, ataleta tafsiri yake kwa lugha yeyote aiwezayo LAKINI afahamu bado inamuwajibikia na kumlazimu kujifunza upesi imkinikavyo.

 (iv)  Mtungamano (Utaratibu) wa matamko yake. Asiyacheleweshe matamko yaliyotangulia na kuyatanguliza yaliyocheleweshwa, bali ayatamke kama yalivyopokewa katika hadithi.

(v)   Mtungamano baina yake (swala ya Mtume) na Tashahudi. Haisihi kuanza  kumswalia Mtume kabla ya kusoma Tashahudi.

KUMSALIA MTUME BAADA YA TASHAHADU YA MWISHO

Hii ndio nguzo ya kumi na moja ya swala. Nguzo hii yaani kumswalia Bwana Mtume, huchukua nafasi mara tu bada ya kukamilka kwa tashahudi na kabla ya kutoa salamu. Hapo ndipo mahala pake nguzo hii.

 Dalili ya swala  ya Mtume.

Kumswalia Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie – ndani ya swala ni katika kulitekeleza agizo na amri ya Allah isemayo

“HAKIKA ALLAH ANAMTEREMSHIA REHEMA MTUME (anaswalia) NA MALAIKA WAKE (wanamuombea dua) BASI, ENYI WAUMINI MSWALIENI (Mtume, muombeeni rehema) NA MUOMBEENI AMANI” (33:56).

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published.