Kitako hiki baina ya sijida mbili ni wajibu kiwepo katika kila rakaa.
Dalili ya kitako hiki:
Kitako hiki kilicho baina ya sijida mbili; ile ya kwanza na ya pili, kimetajwa katika kauli yake Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-iliyo pita:
“…Halafu inuka utulizane hali ya kukaa…” [Rejea dalili za sijida]
Sharti za kitako baina ya sijida mbili: Kumeshurutizwa katika kuswihi kwa kitako hiki, kuchunga mambo yafuatayo:
Akusudie ibada kwa kitako chake hicho na siyo kingine chochote, mithili ya kukaa kwa sababu ya hofu.
Asikitwawilishe (asikirefushe) sana kitako hicho kiasi cha kuzidi muda wa uchache wa Tashahudi.
Kutulizana kiasi cha kuleta Tasbihi moja.