Hii ndio sharti ya tatu miongozi mwa zile sharti nne za kusihi kwa suala. Ili tuweze kuijua vema sharti hii hatuna budi kwanza tuyajue mambo yafuatayo:
i) maana ya utupu
Kisheria utupu ni kila ile sehemu ya mwili ambayo ni wajibu lkuisitiri au ni haramu kuiangalia/kwaangaliwa
ii) Mipaka ya utupu ndani ya swala, ndani ya swala ni lile aneo lote lililo baina ya kitovu na magoti yake. Ni wajibu eneo lote hili lisitiriwe . Mwenyezi MUNGU anasema
“ENYI WANAADAMU CHUKUENI MAPAMBO YENU WAKATI WA KILA SWALA” (7.32)
Muradi wa neno Mapambo ni nguo inayositiri utupu.
Hivi ndivyo ilivyotasfririwa na wataalamu wa fani ya tafsiri. Fahamisho la aya ni kuwa Enyi wanadamu sitirini tupu zenu mnapotaka kuswali.
Imepokelewa hadithi na Said – Al-Khudriy – Allah amuwiye radhi kwamba mtume Rehema na Amani zimshukie amesema
“ Utupu na mwaname ni baina ya kitovu chake mpaka gotini kwake”.
(iii) Kwa upande wa mwanamke: Ni mwili wake wote ukiondoa uso na vitanga vya mikono; Sehemu yote hiyo ya mwili ni wajibu isitiriwe.
Hivyo ndivyo tunavyoelewa kupitia kauli ya Mwenyezi Mungu … wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa VINAVYODHIHIRIKA
Jamhuri ya Mafaqihi wamesema kuwa muradi wa kauli “vinavyodhihirika” ni uso na vitanga
– Imeshurutizwa nguo ya kujisitiri-
– Isiwe nyeupe sana kiasi cha kuonyesha rangi ya mwili mpaka
Mtazamaji akatambua weupe ua weusi wa mwili.
– Isiwe inabana kiasi cha kiliacha finyango la mwili lidhihirike.
Inapendeza kwa muumini kuitekeleza ibada ya swala akiwa katika mavazi twahara , nadhifu, mazuri ayapendayo , akiyavaa roho yake hutua na kuburudika. Tunasema hivi kwa sababu nguo inaweza kuwa twahara lakini sio nadhifu wala nzuri.
iv/. Mipaka ya utupu nje ya swala
i/. Mwanamume mbele ya mwanamume wenziwe na wanawake walio maharimu zake ni sehemu ya mwili iliyo baina kitovu na magoti.
Ama mbele ya wanawake “ajnabiyyat” wa kando na kando wasio maharimu ni mwili wake wote isipokuwa na vitanga kauli yenye kutegemewa katika riwaya ya Ummu Salamah –Allah aminiye radhi –asema
Nilikuwa mbale ya Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie akiwepo na Bi Maimuna (wote hawa ni wakeze) Akaja ibn Ummi Maktuum na (tukio) hilo lilikuwa ni baada ya kuamrishwa Hijaab Mtume akasema : “Jihifadhini nae” tukamwambia : Ewe Mtume wa Allah,YEYE SI KIPOFU, HATUONI NA WALA HATUJUI Mtume akasema :
“Je, na nyinyi ni vipofu, hamuoni” Abuu Daawaoud na Tirmidhiy.
Kwa hiyo haijuzu kwa wanawake “Ajnabiyaat” kuangalia zaidi ya uso na vitanga kwa mwanaume “Ajnabiy”
NA WAAMBIE WAUMINI WA KIKE WAINAMISHE MACHO YAO NA WAZILINDE TUPU ZAO………”(24: 31)
ii/.Ama mwanamke mbele ya wanawake wenziwe waislamu utupu wake ni sehemu yote ya mwili iliyo baina ya uso na kitovu na mbele ya wanawake makafiri ni mwili wake wote ila sehemu inayodhihirika kwa dharura wakati wa kufanya kazi za nyumbani na nyingine kama hizo.
Mbele ya wanaume maharimu zake ni eneo lote lililo baina ya kitovu na magoti.
Yaani inajua kuwa wazi sehemu nyingine ya mwili isiyo hiyo tuliyoitaja mbele ya naharimu zake lakini kwa sharti ya kutokuzuka fitna.
Ikiwa fitna haiaminiki basi si ruhusa Tusome pamoja
WALA WASIONYESHE MAPAMBO YAO ILA KWA WAUME ZAO,AU BABA ZAO, AU BABA ZA WAUME ZAO, AU WATOTO WAO, AU WATOTO WA WAUME ZAO, AU KAKA ZAO, AU WANA WA KAKA ZAO, AU WANA WA DADA ZAO, AU WANAAKE WENZIO ( Waislamu) AU “(24:31)
Ama mbele za wanaume “Ajaanibu” wa kando na kando : wasio waharimu zake ni mwili wake wote Haijuzu kuonyesha sehemu yoyote ya mwili wake mbele yao ila kwa udhuru unaokubalika kisheria haijuzu kwa wanaume hao kumuangalia tusome:
“WAAMBIE WAUMINI WA KIUME WAINAMISHE MACHO YAO (wasitazame yaliyokatazwa ) NA WAZILINDE TUPU ZAO, HILI TAKASO KWAO…………24: 30
Imepokelewa kutoka kwa Bi. Aysha- Allah amuwiye radhi – amesema :
Alikuwa Mtume wa Allah –Rehema na Amani zimshukie- akiswali alfajiri basi wakihudhuria pamoja nae (SWALA) wanawake waumini wakiwa wamejiviringizia nguo zao Kisha ( Ibada ya swala ) hurejea majumbani mwao, hapana yeyote aliyeweza kuwatambua (kutokana na namna walivyovaa) Bukhaariy.
FAIDA HALI/MAENEO AMBAYO KISHERIA INAJUZU KUFUNUA UTUPU NA KUUNGALIA
Inaruhusiwa na sheria kufunua na kuuangalia utupu kwa nyudhuru zifuatazo:
1 Wakati wa kuposa kwa lengo la kuoa. Hapa mposaji anapewa ruhusa na sheria kumtazama mwanamke anayetaka kumposa .
Anachoruhusiwa kuangalia ni uso na vitanga tu na zoezi hili hufanyika mbele ya mawalii wa binti sio faraghani baina ya wawili hao peke yao.Tena ni kuangaliana tu na sio kugusana.
2 Kutazama kwa ajili ya ushahidi au muamala. Ili shahidi akubaliwe
Na mahakama ya Kiislamu kutoa ushahidi dhidi au kwa mwanamke ni lazima
anamtambua. Hapo ndipo sheria inampa ruhusa ya kumuangalia uso tu.
Eneo lingine ni pale anapochanganyika na mwanamke huyo katika shughuli fulani kama vile biashara au ajira pia ni lazima ajue anafanya biashara na nani au anamuajiri/anaajiriwa na nani. Hapa pia anaruhusiwa kutazama uso tu.
3. Kutazama kwa sababu ya kutibu na kufanya dawa. Mwanamke anaumwa, Daktari ni mwanamume na hakuna daktari mwanamke.Sheria inamruhusu daktari kumuangalia popote
Mwanamke huyo kwa lengo la tiba tu. Zoezi hili lifanyike mbele ya maharimu wa mwanamke mgonjwa na sio baina ya wagonjwa na daktari peke yao.
Imepokelewa na Jaabir ibn Abdillah –Allah amuwiye radhi:- kwamba Umu Salamah Allah amuwiye radhi – alimuomba Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie ya kupiga chuku.
Mtume akamuamrisha Abu Twaybah ampige chuku “ Muslim”
CHUKU (cupping) hii ni aina ya tiba inayohusisha ukataji wa mshipa maalum kwa lengo la kutoa damu chafu mwilini
Sharti la nne itatajwa katika somo lijalo. inshaallah