Hapa kinachokusudiiwa ni kile kitako kinachokuwa katika rakaa ya mwisho ya swala, kinachofandamiwa na salamu.
Ni suna iliyothibiti kukaa mkao wa “ Tawarruki” katika kikao hiki cha mwisho .
Huu ni mkao ambao mtu hukalia tako la kushoto na sehemu ya tako la kulia , akaunyoosha mguu wa kulia kama unavyokuuwa katika si jida na kuupitisha ule wa kushoto chini yake.
Imekuja kaatika riwaya ya Abuu humayd :
“ ……………..hata ilipokuwa sijida ambayo ndani yake ndimo imo salamu ( sijida ya mwisho ) huutoa mguu wake wa kushoto na akakaa mkao wa tawarruki kwa kukalia tako lake la kushoto” Abuu Daawound