KATAZO LA WIKI (JUMA LA 88)

Leo ulimwengu mzima unateseka na kupitia katika majanga makubwa, umekumbwa na maradhi mabaya yanayo ambukiza kwa kasi kubwa na kuua kwa halaiki. Familia nyingi leo, watoto wameachwa yatima, wanawake wameachwa wajane, wazazi wanateseka kwa kukosa wa kuwalea.

Yote hayo yanaukumba ulimwengu kutokana na wanaadamu kuutupa muongozo wa Mola Muumba wao na badala yake wakaishi kama watakavyo wao na si kama walivyo pangiwa na Allah. Kumkaidi Allah ni kujitafutia maangamivu, kwani Yeye hakatazi ila hicho alicho kikataza huwa na madhara na wala haamrishi ila kile kilicho na manufaa kwa waja wake.

Kwani ni Yeye ndiye aliye waumba na anawajua fika; lipi linawadhuru na lipi lina faida kwao. Tuacheni zinaa, kwani ndio sababu kubwa ya mengi miongoni mwa maradhi makubwa na mabaya yanayo utesa ulimwengu hivi leo na badala yake tukidhi haja zetu za kimaumbile kwa kupitia mlango wa ndoa tulio funguliwa na Mola wetu.

Haya na tusome kwa nia ya utekelezaji: “WALA MSIKARIBIE UZINZI. HAKIKA HUO NI UCHAFU NA NJIA MBAYA”. Al-Israa [17:32]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *