Kwa nini lakini upuuzie mafundisho ya Mtume wako na kujinyima fursa ya kuhodhi kheri nyingi?! Kwani hujui kuna mambo mengi tu ambayo hayakugharimu chochote na ambayo hayana taklifu hata kidogo, tena mambo hayo hujirudia rudia kila mara?!
Kwani hujapata kusikia ya kwamba Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-amesema: “Hapana muislamu yeyote atakaye tawadha ilivyo ndivyo, kisha akainuka akaswali rakaa mbili. Akimuelekea kwa mbili hizo (Mola wake) kwa moyo wake, ila kutamuwajibikia kuingia peponi”. Muslim [234], Abu Daawoud [169] na Ahmad [04/153]-Allah awarehemu.