Ni wangapi wangapi unao wajua hapo mtaani/kijijini kwako ambao wamesha hangaika Mashariki na Magharibi na kwa kutumia gharama kubwa katika kutafuta kupata japo mtoto mmoja tu, lakini hawajapata. Halafu wewe Mola wako anakuruzuku watoto, kisha wewe unawaua eti kwa kuogopa kushindwa kuwahudumia?! Hapana, hiyo ni dhambi na hatia kubwa mbele ya Mola wako ambaye Yeye ndiye Muumbaji wa watoto hao na ni Yeye pekee ndiye Mruzuku wao na si wewe.
Isome aya hii ya Mola wako na acha mara moja tabia mbaya hiyo na utubu leo kabla ya kesho: “WALA MSIWAUWE WANA WENU KWA KUOGOPA UMASIKINI. SISI TUNAWARUZUKU WAO NA NYINYI. HAKIKA KUWAUA HAO NI KHATIA KUBWA”. Al-Israa [17]:31