KATAZO LA WIKI (JUMA LA 85)

Kwa nini lakini uumie kwa kipato cha mwenzako?! Kwani wewe huamini ya kwamba kipato alicho nacho ni riziki aliyo pewa na Mola wake kwa hekima anazo zijua Yeye Mwenyewe?!

Kwa nini hutaki kukubali kuwa hicho ulicho nacho wewe pia kinatokana na mgao wa riziki wa Mola wako?! Usiumie bure hata ukapata dhambi kwa kile kinacho milikiwa na kugawiwa na Mmiliki wa hazina zote za mbinguni na ardhini, lako wewe ni kujitahidi katika sababu za kupatia riziki na Allah ataibariki juhudi yako hiyo.

Fanya hivyo huku ukitia akilini mwako ya kwamba: “HAKIKA MOLA WAKO MLEZI HUMKUNJULIA RIZIKI AMTAKAYE, NA HUMPIMIA AMTAKAYE. HAKIKA YEYE KWA WAJA WAKE NI MWENYE KUWAJUA NA KUWAONA”. Al-Israa [17:30]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *