KATAZO LA WIKI (JUMA LA 82)

Swala ni amri ya Mola Muumba wako, anataka umsujudie kila siku sijida thelathini na nne za faradhi ukiachilia mbali zile za sunna. Kwa nini ujitoe kwenye jina zuri alilo kupa Allah “waja wangu”, kwa kukataa kuswali?! Ukiwa sio mja wa Allah kwa sababu ya kukataa kumsujudia ndani ya swala, unafikiri utakuwa mja wa nani mwingine kama si shetani?!

Acha uvivu na wala usigubikwe na ajizi, anza kuswali leo ili upate heshima ya kuwa miongoni mwa waja wa Allah, haya na tupulike: “WAAMBIE WAJA WANGU WALIO AMINI, WASHIKE SWALA, NA WATOE KATIKA TULIVYO WARUZUKU, KWA SIRI NA DHAAHIRI, KABLA HAIJAFIKA SIKU ISIYO KUWA NA BIASHARA WALA URAFIKI”. Ibraahim [14]:31

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *