KATAZO LA WIKI (JUMA LA 81)

Kwa nini hufikiri kwanza kabla ya kutenda/kufuata?! Kwa nini umekuwa ni muhanga wa kuzolewa na ufuataji wa kibubusa?! Kwa nini unakuwa mtumwa wa viongozi/watu wakubwa, kila wanalo sema wewe unafuata tu kikondoo kondoo pasina kubali (kujali) Mola wako ametoa muongozo gani katika hilo unalo lifuata kwa kuwatii wakubwa hao?!

Hao unao wafuata leo kwa maslahi duni na ya mpito, watakukana kesho mbele ya mahakama adilifu ya Mola wako, hebu na tuzingatie: “NA WOTE WATAHUDHURIA MBELE YA ALLAH. WANYONGE WATAWAAMBIA WALIO TAKABARI: SISI TULIKUWA WAFWASI WENU; BASI HEBU HAMTUONDOLEI KIDOGO HIVI KATIKA ADHABU YA ALLAH? WATASEMA: LAU ALLAH ANGELI TUONGOA BASI HAPANA SHAKA NASI TUNGELI KUONGOENI. NI MAMOJA KWETU TUKIPAPATIKA AU TUKISUBIRI; HATUNA PA KUKIMBILIA”. Ibraahim [14]:21

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *