KATAZO LA WIKI (JUMA LA 80)

Ubakhili ni wa nini na mpaka lini huo ubakhili wako. Tangu umeamua kuwa bakhili mpaka leo umepata faida gani?! Acha ubakhili, kwani kuwa bakhili ni kujinyima mwenyewe fursa ya kuipata pepo.

Umepewa na Allah, kwa nini basi wewe hutaki kuwapa waja wa Allah sehemu ndogo tu katika vile ulivyo ruzukiwa?! Acha ubakhili mara moja kwa kuwaidhika na kauli ya Mmiliki wa khazina zote za mbingu na ardhi: “KABISA HAMTAFIKIA WEMA (Pepo) MPAKA MTOE KATIKA VILE MNAVYO VIPENDA. NA KITU CHOCHOTE MNACHO KITOA, BASI HAKIKA ALLAH ANAKIJUA”. Aali Imraan [03]:92

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *