KATAZO LA WIKI (JUMA LA 79)

Dini yako haina thamani; haiuziki kwa chochote. Dini yako ndio kitu ghali mno unacho miliki, kwa nini basi unazipotoa aya za Mola wako kwa maslahi ya wanasiasa au kwa kujipendekeza kwa wenye madaraka na uwezo wa kimali?! Acha, hilo litakunyima kupata kheri Akhera na litakupatia adhabu chungu.

Hebu jihurumie kwa maslahi na manufaa yako mwenyewe, zingatia: “Hakika wanao uza ahadi ya Allah na viapo vyao thamani ndogo (dunia), hao hawatakuwa na sehemu ya kheri yoyote Akhera, wala Allah hatasema nao wala hatawatazama Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa, nao watapata adhabu chungu”. Aali Imraan [03]:77

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *