Acha ajizi na uvivu, kwa nini lakini unajinyima mwenyewe fursa ya kujizolea thawabu lukuki kwa amali ndogo kabisa, ambayo wewe unaiweza pasina kukuletea mashaka?! Hivi ni kweli wewe unashindwa kuswali rakaa mbili nyepesi kila unapo chukua udhu?! Hapana, hushindwi bali unachezewa na shetani ili kukuzuia kujiongezea mafao yako ya akhera.
Hebu msikilize vema Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-namna anavyo zielezea rakaa mbili baada ya udhu, halafu ndio uamue kuswali au kutokuswali kila baada ya udhu: “Atakaye tawadha kiukamilifu, kisha akaswali rakaa mbili, akamuelekea kwazo (mbili hizo Mola wake) kwa moyo wake na uso wake, (huyo) imemuwajibikia Pepo”. Nasaai [151], Muslim [234], Abu Daawoud [169] & Ahmad [04/157]-Allah awarehemu.