KATAZO LA WIKI (JUMA LA 75)

Si ustaarabu, si uungwana na wala sio mafundisho ya Uislamu, kwa nini lakini ushike utupu (uchi) wako wa mbele au wa nyuma kwa mkono wako wa kulia?! Kumbuka lakini, mkono huo ndio unao utumia katika kula chakula, huo huo ndio unao utumia katika kusalimiana na wapendwa wako, kwa nini basi uutumie katika mahala panapo toka haja?! Usifanye hivyo, hilo limekatazwa na mwanaadamu aliye bora kuliko wewe; Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-ametuambia: “Kabisa kabisa, asishike mmoja wenu dhakari yake kwa mkono wake wa kulia wakati anapo kojoa na wala asipanguse chooni kwa mkono wake wa kulia na wala asipumulie ndani ya chombo”. Bukhaariy [153], Muslim [267], Abu Daawoud [31], Nasaai [34], Tirmidhiy [15], Ibn Maajah [310] & Ahmad [05/296]-Allah awarehemu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *