KATAZO LA WIKI (JUMA LA 73)

Kwa nini ujidhuru eti kwa sababu tu ya kuacha utaratibu na mafundisho mepesi na rahisi mno ya Uislamu ambayo yanakuelekeza namna ya kujikinga dhidi ya mashetani wanao kaa vyooni?!

Ni mara ngapi umepata kusikia watu wameanguka mweleka humo vyooni?! Ingia na toka chooni kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu ili upate kusalimika na shari ya mashetani waovu ambao maskani yao ni mahala pachafu, haya na tumsikilize Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-akituelekeza namna ya kujikinga na shari za mashetani waovu hao:

“Hakika humu muhala mwa kukidhi haja, huingiwa na majini na mashetani. Atakapo taka mmoja wenu kuingia chooni na aseme: Audhubillaahi minal-khubuthi wal-khabaaithi – Ninajikinga kwa Allah dhidi ya mashetani wa kiume na mashetani wa kike”. Abu Daawoud [06], Ibn Maajah [296] & Ahmad [04/369]-Allah awarehemu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *