KATAZO LA WIKI (JUMA LA 71)

Mbona unakosa haya, kwa nini lakini huoni aibu, huoni vibaya kujivunjia heshima na kujidharaulisha mbele za watu?! Ni kwa lipi hasa hata uthubutu kuufanya mwili wako kuwa ni maonyesho kwa kila aonaye?! Haifai na imekatazwa kujisaidia au kuoga hadharani au mahala ambapo unaonekana na kila apitaye, jisitiri unapo kidhi haja zako na kumbuka kwamba: Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-alimuona mtu akioga kwenye bafu lililo wazi pasina shuka (kikoi), akapanda juu ya mimbari, akamuhimidi Allah na kumsifia, kisha akasema: “Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye haya mno na Mwenye kusitiri mno, basi atakapo oga mmoja wenu na ajisitiri”. Abu Daawoud [4012], Nasaai [406] & Ahmad [04/224]-Allah awarehemu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *