KATAZO LA WIKI (JUMA LA 70)

Kwa nini uwe muflisi akhera, kwa nini unafanya amali ili uonekane na watu, ili usifiwe na watu?! Kwani hao ndio watakao kupa jazaa ya matendo yako hayo?! Hapana, usifanye hivyo, hakikisha kila ulitendalo liwe ni kwa ajili ya kumkusudia Allah pekee, kwani ni Yeye tu ndiye anayejua ukweli wa mja katika matendo yake hayo, na ni Yeye tu ndiye Mlipaji. Tuzingatie pamoja: Imepokewa ya kwamba bedui mmoja alikuja kwa Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-akasema: Hakika mtu hupigana ili apate kutajwa, na hupigana ili apate kusifiwa, na hupigana ili apate ngawira, na hupigana ili uonekane ushujaa wake. Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-akasema: “Atakaye pigana ili neno la Allah (dini) ndilo liwe juu kabisa, huyo ndiye yuko katika njia ya Allah”. Abu Daawoud [2517], Nasaai [3136], Ibn Maajah [3136] & Ahmad [04/402]-Allah awarehemu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *