Eti kwa kuwa umeswali sana miaka mingi, umefunga sana faradhi na sunna, umehiji na kufanya umra mara nyingi, umejenga misikiti na madrasa, umetoa sana sadaka, na … na …. Basi ndio ujione kuwa wewe ni mtu wa peponi, hapana huko ni kughurika, hatuingii peponi kwa wingi wa amali. Hebu tega sikio lako upulike: “Fanyeni yaliyo sahihi na yatekelezeni na ikupateni bishara njema. Kwani hakika ya mambo yalivyo, hakuna yeyote atakaye ingizwa peponi na amali zake. (Maswahaba) wakauliza: Hata wewe, ewe Mtume wa Allah! Akajibu: Hata mimi, ila tu kama Allah atanifunika kwa msamaha na rehema zake”. Bukhaariy [08/474]-Allah amrehemu.