KATAZO LA WIKI (JUMA LA 69)

Umefanya uliyo yafanya ndani ya pazia la usiku, umemuasi Mola Muumba wako, umejidhulumu nafsi yako, umevunja heshima za watu na kudhulumu haki zao. Mola wako amekusitiri na pazia hilo la usiku, haya iweje tena wewe baada ya kupambazuka unayaanika hadharani yale uliyo yatenda usiku miongoni mwa maasi?! Badala ya kuitumia fursa ya mchana kumuomba maghufira Mola wako, wewe ndio unapita kujisifu ili iweje?! Acha, tena acha mara moja, hilo halifai. Hebu itafakari kauli hii ya Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie: “Umati wangu wote utasamehewa makosa yao ila wale wanao yaweka hadharani waliyo yatenda faraghani. Na hakika miongoni mwa kutokujali ni mtu kutenda tendo ovu usiku, kisha anapambazukia na ilhali Allah amekwisha muhifadhi, yeye anasema (kuwahadithia watu): Ewe fulani! Jana nimefanya kadhaa na kadhaa. Na ilhali Mola wake amemuhifadhi usiku kucha, halafu anapambazukiwa anaiondoa mwenyewe stara aliyo iweka Allah”. Bukhaariy [08/95]-Allah amrehemu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *