KATAZO LA WIKI (JUMA LA 63)

Ni mizani gani inayo kufanya ukipe nafasi kubwa na ya kwanza kile utakacho kiacha na kile kitakacho kuwa na wewe popote pale utakapo kuwepo unakipa nafasi ndogo na ya mwisho?! Kwa nini unashughulishwa mno na mali na familia yako kiasi cha kusahau kutenda amali zitakazo kunufaisha hata baada ya kutengana nao?! Kwani wewe hutambui ya kwamba: “Vinamfuata maiti vitu vitatu na (katika vitatu hivyo) vinarudi viwili na kinasalia pamoja nae kimoja. Inamfuata (kwenda makaburini) familia yake, mali yake na amali (matendo) zake. (Baada ya maziko) inarudi familia yake na mali yake na inasalia amali yake”. Bukhaariy [08/521]-Allah amrehemu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *