Kwa nini lakini ulimi wako unakuwa mwepesi mno katika mambo ya kipuuzi na unakuwa mzito mno katika kufanya dhikri?! Kwa nini huishukuru neema ya ulimi kwa kumdhukuru aliye kupa neema hiyo, kisha akakulipa ujira maridhawa?! Kwani wewe hujasikia ya kwamba Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-amesema: “Atakaye sema: Laa ilaaha illal-laahu wahdahu laa shariika lahuu, lahul-mulku walahul-hamdu wahuwa ‘alaa kulli shai-in qadiiru, kila siku mara mia moja. (Tasbihi hizo) zitakuwa kwake sawa na kuacha huru watumwa kumi, na ataandikiwa mema mia na kufutiwa dhambi mia. Na zitakuwa kinga kwake kumkinga na shetani katika siku yake hiyo mpaka jioni. Hakuna yeyote atakaye lifanya lililo bora zaidi yake, isipokuwa atakayefanya zaidi ya alivyo fanya yeye”. Bukhaariy [08/514]-Allah amrehemu.