KATAZO LA WIKI (JUMA LA 60)

Hivi bado tu haujafika wakati wa kurejea kwa Mola wako, ukamdhukuru, ukamuomba maghufira na ukatubia kwa mengi maovu uliyo yatenda?! Kumbuka: “Allah Aliyetukuka anasema: Mimi niko vile atakavyo nidhania kuwa mja wangu, nami niko pamoja naye pale atakapo nikumbuka. Atakapo nikumbuka nafsini mwake, nami nitamkumbuka nafsini mwangu. Na atakapo nikumbuka penye wengi, nami nitamkumbuka penye wengi walio bora zaidi yao. Na kama atajikurubisha kwangu kwa shubiri, nami nitajikurubisha kwake kwa dhiraa. Na akijikurubisha kwangu kwa dhiraa, nami nitajikurubisha kwake kwa pima. Na kama atanijia anatembea, nami nitamjia mbio”. Bukhaariy [09/502]-Allah amrehemu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *