KATAZO LA WIKI (JUMA LA 68)

Maswahaba-Allah awawiye radhi-walipigana jihadi kwa ajili ya dini hii, wakauawa, wakapata majeraha na vilema vya kudumu. Leo wewe pia unayo nafasi ya kupata thawabu za jihadi, kwa nini huipatilizi nafasi hiyo?! Kwani wewe hujui ya kwamba: “Anaye wapatia mahitaji yao wajane na masikini, ni sawa na anayepigana jihadi katika njia ya Allah. Au ni kama anaye simama usiku kufanya ibada na anaye funga mchana kutwa”. Bukhaariy [07/265]-Allah amrehemu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *