Unalalamika maisha yamekuwa magumu na kumbe ugumu huo unausababisha wewe mwenyewe kutokana na matendo yako mabaya! Ni lipi khasa linalo kufanya uwe mbali na ndugu zako, ni elimu uliyo nayo ndio inayo kufanya uwaone wao wajinga na si stahiki yako, ndio sababu unawatenga?! Ni kipato ulicho nacho, ndicho kinacho kupa kiburi cha kutokuchanganyika na ndugu zako masikini?! Au tuseme ni madaraka/cheo ulicho nacho, ndicho kinacho kupelekea kuwaona kinyaa?! Koma, matendo hayo mabaya yanaweza kuifinya riziki yako na kuupunguza umri wako. Hebu yazingatie maneno haya ya Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie: “Yule anaye taka kukunjuliwa riziki yake au kuzidishiwa umri wake, basi na auunge udugu wake”. Bukhaariy [03/281]-Allah amrehemu.