KATAZO LA WIKI (JUMA 59)

Wewe huna matendo mema, basi kwa nini hujitahidi angalau kuwapenda watu wema?! Kwani hujui ya kwamba ukiwapenda watu wema, utatiwa katika kundi lao hata kama huna matendo mema kama yao?! Sikiliza: Aliulizwa Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie: Vipi ikiwa mtu anawapenda watu lakini hawezi kuyafikia matendo yao mazuri na kuwa kama wao? Akajibu (Mtume): “Mtu yuko pamoja (ataendelea kuwa pamoja) na aliye mpenda”. Bukhaariy [08/191]-Allah amrehemu.

Allah amrehemu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *