KATAZO LA WIKI

Acha ajizi na uvivu, baada ya kutekeleza yale aliyo kufaradhishia Mola Muumba wako, usipitwe na fursa ya kujikurubisha kwake kupitia amali mbali mbali za Sunna. Jipendekeze kwa Mola wako ili upendwe naye na akupendezeshe kwa watu wote, usikubali kupitwa na fursa hiyo. Tusome:
“Hakika Allah Aliyetukuka anapompenda mja, humwita Jibrilu akamwambia: Hakika Allah amempenda fulani, basi nawe mpende. Jibrilu atampenda (mja huyo kwa mapenzi ya Allah), kisha Jibrilu atalingana mbinguni kwa kusema: Hakika Allah amempenda fulani nanyi mpendeni. Basi apendwe na wa mbinguni na awekewe kukubalika kwa wa ardhini”. Bukhaariy [09/577]-Allah amrehemu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *