Maana ya asili ya neno janaba ni umbali. Hivi ndivyo ilivyotumika ndani ya Qur-ani :
“….BASI YEYE AKAMUANGALIA KWA MBALI BILA WAO KUJUA” [28:11].
Kadhalika neno janaba linachukua maana ya MANII yatokayo kwa mchupo kama libebavyo maana ya JIMAI (tendo la ndoa).
Kwa maana tunaposema Fulani ni mwenye janaba/ana janaba tunamaanisha si twahara/hana twahara kutokana na kutokwa na manii au kujamiiana yaani kutokana na kufanya tendo la ndoa.