HAY-AAT

Maana:           Hizi ni zilizomo ndani ya swala ambazo hakukusuniwa kuleta sijida mbili za kusahau iwapo mwenye kuswali ataacha kuzileta.

1.      Kunyanyua mikono wakati wa kuleta Takbiyra ya kuhirimia, kwenda na kutoka rukuu.

 Namna ya utekelezaji wa suna hii ni mtu kuinyanyua mikono yake na kuyaelekeza kibla matumbo ya vitanga vya mikono hali ya kuvikunjua vidole. Akivielekezea vidole gumba vyake ndewe za masikio yake.

 Suna hii ya unyanyuaji wa mikono mwanzoni mwa swala imepokelewa na maswahaba khamsini, miongoni mwao ni wale kumi walobashiriwa pepo na Bwana Mtume na hakuna Imamu hata mmoja aliyeipinga suna hii.

i./ Imepokelewa kutoka kwa Ibn Umar Allah awawiye radhi amesema:

Nilimuona Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie akiifungua swala kwa takbiyrah, akainyanyua mikono yao wakati alipoleta takbiyrah mpaka ikawa welekea wa mabega (mkabala) yake.

Na anapoleta takbiyrah ya kwenda rukuu hufanya hivyo hivyo. Na anaposema:

SAMI’A-LLAHU LIMAN HAMIDAH

hufanya hivyo hivyo na akasema RABBANAA WALAKAL-HAMD Wala hafanyi hivyo wakati anaposujudu wala wakati anapokimyanyua kichwa chake kutoka sijida”. Bukhaariy na Muslim

ii./ Imepokelewa na Imamu Aliy Ibn Abiy Twaalib Allah amridhie kwamba:

“Alikuwa Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie anaposimama kuswali swala ya fardhi, huleta takbiyrah na akainyanyua mikono yake mkabala wa mabega yake.

Hufanya kama hvi anapomaliza kisomo chake (cha Al-hamdu na sura) na akataka kurukuu.

Na hufanya hivyo anapoinuka kutoka rukuu. Wala hainyanyui mikono yake katika sehemu ye yote ya swla yake akiwa amekaa.

Na anapoinuka kutoka katika sijida mbili hizo (kuja kuanza rakaa nyingine) kadhalika huinyanyua mikono yake na akakabiri (akaleta takbiiyrah)” Bukhaariy, Tirmidhiy, Abuu Daawoud na Ahmad., kutokana na hadithi sahihi hizi inatudhihirikia kwamba ni suna kunyanyua mikono kwa sura/namna tuliyoieleza katika sehemu nne ndani ya swala:-

1.   Wakati wa Takbiyra ya kuhirimia swala.

2.   wakati wa kwenda rukuu

3.   wakati wa kuinuka kutoka rukuu (itidali) na

4.   wakati wa kutoka sijida ya pili kuja Qiyaamu (kisimamo cha rakaa nyingine)

2.  Kuweka mkono wa kulia juu ya ule wa

Baada ya kuhirimia swala, kuleta takbirah na kuinua mikono kama ilivyobainishwa na hadithi, ni suna kuweka mkono wa kulia juu ya ule wa kushoto.

Namna yake ni kuweka kitanga cha  mkono wake wa kulia juu ya mgongo wa kitanga cha kushoto chini ya kifua na juu ya kitovu.

Haya yanatokana na riwaya iliyopokelewa kutoka kwa Wail Ibn Hujri Allah amuwiye radhi kwamba yeye alimuona Mtume wa Allah akiinyanyuua mikono yake anaopingia ndani ya swala — kasha akawkea mkono wake wa kulia juu ya ule wa kushoto.” Muslim.

3.      Kuangalia mahala anaposujudu

Ni karaha kwa mwenye kuswali kuyapepesa macho yake huku na kule ndani ya swala.

Bali ni suna adumishe kuangalia chini mahala anaposujudu ila wakati wa tashahudi. Katika tashudhi suna in kukiangalia kidole cheke cha shahada.

Imepokelewa kutoka wa Anas Ibn Maalik Allah amuwiye radhi kwamba amesema mtume wa Allah Rehema na Amanui zimshukie:

“Wana nini watu wanaonyanyua macho yao kutazama juu ndani ya swala zao, wakomeke (waache) kufanya hivyo au yatangyakuliwa yatanyakuliwa macho yao.” Bukhaariy na Muslim. Zote dalili kubwa katika suna zote hizi ni suala zima la kumfuata mtume, kwani ndiye aliyesema: “Swalini kama mlivyoniona nikiswali.”.

Na hivyo ndivyo alivyoonekana Mtume wa Allah akiswali na kunukuliwa kwetu na maswahaba wake.

4.  Kusoma dua ya ufunguzi wa swala;

Alikuwa Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie akimuomba Mola wake kwa aina mbalimbali za dua baada ya takbiyrah ya kuhirimia na kabla ya kuanza kusoma Suuratil Faatiyhah (Al-hamdu).

Miongoni mwa dua alizokuwa akiziomba ni ile iliyomo katika riwaya iliyopokelewa na Aliy Ibn Abiy Twaalib Allah amuwiye radhi kwamba Mtume wa Allah Rehema na amani zimshukie alikuwa anaposimama ndani ya swla shukie alikuwa anaposmama ndani ya swala husema:

 “WAJJAHTU WAJHIYA LILLADHI FATARASSAMAWATI WAL-ARDHI, HANIIFAN WAMAA ANA MINALMUSHRIKIIN. INNA SWALAATIY WANUSUKIY WAMAHYAAYA WAMAMAATIY LILLAHI RABBIL-‘ALAMIIN, LAA SHARIKA LAHU WABDIHALIKA UMIRTU WA ANA MINAL-MUSLIMIIN” Muslim

 Kutokana na hadithi hii na nyinginezo imethibiti kuwa ni suna kusoma dua ya ufunguzi wa swala katika swala ya fardhi au ile ya suna.

Suna hii inawahusu wote, Imamu, maamuma na hata yule mwenye kuswali pekee. Mahala pa kuilete suna hii ni kabla ya kuanza kuisoma suuratil Faatihah.

Akianza tu kuisoma, basi suna hii itakuwa imefutu na hatakiwi kuikata Alhamdu na kurudi kuisoma dua hii ya ufunguzi hata kama alifanya hivyo kwa kukosea au kusahu.

Pia ni vema ikakumbukwa kwamba ni suna kuleta dua ya ufunguzi katika swala ya maiti wala katika swala ya fardhi wakati utakapodhiki/utakapokuwa finyu kiasi cha kuchelea kutoka kwa wakati

 5. Istiaadha.

Ni suna thabiti kutoka kwa Mtume, mwenye kuswali alete “Istaadha” baada ya kumaliza kusoma dua ya ufunguzi na kabla ya kuanza kusoma suuratil aatihah. Istiaadhah ni kusema.

AUDHU BILLAHI MINASHHAITAANIR-RAJIIM kwa kulitekeleza agizo la Allah:

“NA UKITAKA KUOSMA QURANI PIGA AUDHU (kwanza, jikinge) KWA ALLAH (akulinde) NA SHETANI ALIYEFUKUZWA (katika rehema yake Allah).” [16 : 98]

 6. Kujihirisha na kusirisha kisomo katika sehemu zake:

Sehemu/mahala ambamo ni suna kujihirisha kisomo (kusoma kwa sauti yenye kusikika) ni:-

i.    Rakaa mbili za swala ya Alfajiri.

Hili linatokana na hadithi ya Ibn Abbaas Allah amuwiye radhi alipokuwa akisimulia kuhudhuria kwa majini na kuisikiliza Qurani kwa Mtume Rehema na Amani zimshukie sehemu ya hadithi inasema Na ilhali yeye (Mtume) akiwaswalisha maswahaba wake swalatil fajri, waliposikia (majini) Qur-ani hiyo (iliyokuwa ikisomwa na Mtume] walikaa kusikiliza.” Bukhaariy na Muslim

Imepokelewa na Ubaadah Ibn Swaamit Allah amuwiye radhi tulikuwa nyuma ya Mtume Rehema na Amani zimshukie katika swala ya Alfajiri, kisomo kikamuwiya uzito (akakwama).

Alipomaliza swala akasema: “Huenda nyinyi mnasoma nyuma ya imamu wenu.” Akasema (ubaadah) tukasema ewe Mtume wa Alah, ndiyo wallah. Akasema:

 “Msisome ila Ummul Qurani (Suuratul faatihah), kwani hana swala asiyeisoma.” Abuu Daaoud na Nasaai. Na katika riwaya nyingine:

“Msisome cho chote katika Qurani nitakapojihirisha kusoma (Qurani) ila (someni) Ummul Qurani

Hadithi hizi zinafahamisha kwamba Bwana Mtume Rehema na Amani zimshukie alikuwa akijihirisha kisomo chake (cha Qurani) kiasi cha kusikiwa na maamuma wake.

ii.   Rakaa mbili za mwanzo za swala za magharibi na Ishaa.

Haya ni kwa mujibu wa riwaya iliyopokelewa kutoka kwa Baraa Allah amuwiye radhi amesema Nilimsikia Mtume Rehema na Amani zimshukie akisoma: “Wattiyn waz-zaytuun”.

Katika swala ya Ishaa. Na sikupatapo kumsikia mtu mwenye sauti nzuri kuliko yeye” Bukhaariy na Muslim

iii.  Swala za Ijumaa, Eid mbili, ya mfunguo mosi na mfunguo tatu, swala ya kupatwa kwa mwezi, swala ya kuomba mvua, swala ya taraweh, swala ya witri ya Ramadhan.

Humu ndimo mahala ambamo ni suna mtu kusoma Qurani kwa sauti ndani ya swala kwa ushahidi wa hadithi nyingi sahihi zilizothibiti kutoka kwa Bwana mtume sehemu nyingine zote ambazo hatukuzitaja atasoma kwa kusirisha (bila ya kutoa sauti).

Imepokelewa kutoka kwa khabaab Allah amuwiye radhi alipoullizwa na muulizaji: Je, Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie alikuwa akisoma katika swala ya Adhuhuri na Alasiri akajibu. Nido tukamuuliza tena mlikuwa mkilijuaje hilo (kwamba yeye anasoma). Akajibu kutokana na kuchezacheza kwa ndevu zake Bukhaariy.

7.  Kuitikia Aamiyn inaposomwa suuratil faatihah

uitikjiaji huu ni kuifuatishia kauli ya Allah iliyoko mwishoni mwa suuratil faatihah na tamko “Aaamiyn.”

Kuitikia “Aaamiyn” mara tu baaada ya kumaliza kusoma suuratil Faatihah ni suna kwa kila anaye swali, Imamu, maamuma na mwenye kuswali pekee.

Ataitikia kwa sauti katika swala inayoswaliwa kwa kutolewa sauti na bila ya kutoa sauti katika swala iswaliwayo bila ya kutolewa sauti.

Na maana ya kiitikio hiki “Aamiyn” ni tukubalie itupokelee swala/dua yetu hii ewe Bwana Mlezi wetu.

Uitikiaji huu wa “Aaamiyn” tunaupata kutokana riwaya zilizopokelewa na Abuu Hurayrah Allah amuwiye radhi amesema “Atakapoitikia Imamu “Aaamiyn” nanyi itikieni, kwani mwenye kuwafikiana Aamiyn yake na Aamiyn ya malaika hughufiriwa dhambi zake zilizotangulia.” Bukhaariy na Muslim.

 Amesema Abuu Huayrah alikuwa Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie anaposoma WALADHWAALIIN  husema/huitikia: Aaamiyn, mpaka huweza kumsikia wanaomfuatia, yaani watu wa safu ya kwanza.Abuu Daawoud.

 Imamu Ibn Maajah akazidisha katika riwaya yake: “— Na msikiti mzima ukaripuka kwa kuitikia Aaamiyn.”

 8.  Kusoma sehemu ya Qur-ani baada ya suuratil Faatihah:

suna hii huthibiti kwa kusoma sura ye yote ndani ya Qur-ani hata ikiwa ni fupi au kwa kusoma aya tatu zenye kufuatana.

Suna hii hutekelezwa katika rakaa mbili za mwanzo za kila swala, kwa imamu na mwenye kuswali pekee (munfarid).

Pia suna hii humuhusisha maamuma katika swala inayoswaliwa bila ya kutoa sauti au, maamuma anapokuwa mbali, mahala ambapo hakisikii kisomo cha imamu wake.

 Ni suna kwa mwenye kuswali asome “sura ndefu kiasi” kama vile Hujuraat {49}, Rahmaan {55} na kadhalika katika swala za Alfajiri na Adhuhuri, katika swala za alasiri na Ishaa, asomo “Sura za kati na kati” kama vile As-shamshi {91}, Al-layli {92} na kushuka chini, katika swala ya Maghribi asome “sura fupi” kama vile Ikhalaaswi {112}.

 Hivi ndivyo tunavyojifunza kutokana na hadithi iliyopokelewa na Sulayman Inb Yasaari nae akipokea kutoka kwa Abuu Hurayrah Allah awawiye radhi amesema Sijapata kuswali nyuma ya mtu yeyote swala inayoshabihiana kabisa na ya Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie kuliko mtu Fulani.

Tuliswali nyma ya mtu huyu (akisoma sura ndefu) katika rakaa mbili za mwanzo za swala ya Adhuhuri na kaikhafifisha katika zile mbili nyingine. Na akikhafifisha (akisoma sura fupi) katika swala ya Alasiri na akisoma katika swala ya Maghribi sura fupi.

Na akisoma katika swala ya Ishaa “Was-shamsi wadhuhaa” na mfano wake, na katika swala ya sub-hi akisoma sura mbili ndefu.” Nasaai

 Faida

i./ Ni suna kusoma katika swala ya sub-hi ya siku ya Ijumaa Suuratis Sajidah (32) katika rakaa ya kwanza na Al-insaan (76) katika rakaa ya pili.

Hili linapatikana katika riwaya ya Abuu Hurayrah Allah amuwiye radhi amesema: Mtume Rehema na Amani zimshukie alikuwa akisoma katika swala ya Alfajiri ya siku ya Ijumaa ALIF LAAM MIIM TANZIIL As-sajidah na Al-insaan. Bukhaariy na Muslim

 ii./ Kadhalika ni suna katika swala zote kuirefusha rakaa ya kwanza kuliko ile ya pili kama ilivyopokelewa: “mtume Rehema na Amani zimshukie alikuwa akirefusha katika rakaa ya kwanza na kufupisha katika rakaa ya pili.” Bukhaariy na Muslim

HAY-AAT

Maana:           Hizi ni zilizomo ndani ya swala ambazo hakukusuniwa kuleta sijida mbili za kusahau iwapo mwenye kuswali ataacha kuzileta.

1.      Kunyanyua mikono wakati wa kuleta Takbiyra ya kuhirimia, kwenda na kutoka rukuu.

 Namna ya utekelezaji wa suna hii ni mtu kuinyanyua mikono yake na kuyaelekeza kibla matumbo ya vitanga vya mikono hali ya kuvikunjua vidole. Akivielekezea vidole gumba vyake ndewe za masikio yake.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *