HADITHI YA WIKI (JUMA LA 88)

Imepokewa kutoka kwa Jaabir bin Abdillah – Allah awawiye radhi – ya kwamba Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-amesema: “Nimepewa mambo matano ambayo hajapata kupewa yeyote kabla yangu; Nimenusuriwa kwa (adui yangu kutiwa) khofu mwendo wa mwezi mzima, na nimefanyiwa ardhi (yote) kuwa ni mahala pa kuswalia, basi popote pale mtu katika uma wangu itakapo mdiriki swala, basi na aswali. Na nimehalalishiwa ngawira na haijahalalishwa kwa yeyote kabla yangu, na nimepewa shafaa (uombezi). Na Mtume alikuwa anapelekwa kwa kaumu yake tu nami nimepelekwa kuwa Mtume kwa watu wote (ulimwengu mzima”. Bukhaariy [335], Muslim [521], Nasaai [430] na Ahmad [03/304]-Allah awarehemu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *