Imepokewa kutoka kwa Uthmaan bin Affaan-Allah amuwiye radhi-kutoka kwa Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-amesema: “Atakaye ukamilisha udhu kama alivyo amrishwa na Allah, basi swala tano (anazo ziswali kwa udhu huo), ni kafara (ya kufuta madhambi) yaliyo baina yake (swala na swala nyingine)”. Nasaai [145], Ahmad [01/66], Bukhaariy [160] na Muslim [227] – Allah awarehemu.