HADITHI YA WIKI (JUMA LA 83)

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira-Allah amuwiye radhi-ya kwamba Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-amesema: “Atakapo tawadha mja muislamu – au muumini – akaosha uso, litatoka usoni mwake pamoja na maji kila dhambi alilo litazama kwa macho yake – au pamoja na tone la mwisho la maji. Na atakapo osha mikono yake, litatoka mikononi mwake pamoja na maji kila dhambi alilo litenda kwa mikono yake – au pamoja na tone la mwisho la maji. Na atakapo osha miguu yake, litatoka miguuni mwake pamoja na maji kila dhambi lililo endewa na miguu yake – au pamoja na tone la mwisho la maji. Mpaka atoke (baada ya kumaliza kutawadha) akiwa ametakasika na madhambi”. Muslim [244], Tirmidhiy [02], Ahmad [02/303] na Ibn Maajah-Allah awarehemu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *