“Twahara ni nusu ya Imani, na Alhamdulillaah inajaza mizani (ya amali za mja). Na Sub-haanallah na Alhamudilillaah zinajaza – au inajaza kilichopo baina ya mbingu na ardhi. Na swala ni nuru, na sadaka ni hoja, na subira ni nuru na Qur-ani ni hoja ya kukunusuru au dhidi yako. Watu wote wanadamka, basi mwenye kuiuza nafsi yake, ataiacha huru au ataingamiza”. Muslim [223], Tirmidhiy [3517], Ibn Maajah [280] na Ahmad [05/343]-Allah awarehemu.