“Siku bora zaidi iliyo chomozewa na jua ni siku ya Ijumaa; ndani ya siku hiyo Allah alimuumba Adam (baba yetu), ndani yake alimkubalia toba yake, ndani ya siku hiyo akiteremshwa ardhini kutoka mbinguni na ndani ya siku hiyo alifariki. Na ndani ya siku hiyo kitasimama Kiyama na hakuna kiumbe chochote katika usiku wa kuamkia Ijumaa ila huwa makini mpaka lichomoze jua kwa kuogopa huenda ikawa ndio siku ya Kiyama, isipokuwa majini na watu (wao hawana khabari). Na ndani yake (siku hiyo kila Ijumaa), imo saa (muda mfupi) haipati mja muislamu akamuomba Allah chochote ila humpa kitu hicho”.