“Atakapo tawadha mja muislamu – au muumini – akaosha uso wake, basi hutoka pamoja na maji hayo kila dhambi aliyo ipata kwa kuangalia kwa macho yake – au pamoja na tone la mwisho la maji hayo. Na atakapo osha mikono yake, basi hutoka pamoja na maji hayo kila dhambi aliyo ifanya kwa mikono yake – au pamoja na tone la mwisho la majihayo . Na atakapo osha miguu yake, hutoka pamoja na maji hayo kila dhambi iliyo fanywa na miguu yake – au pamoja na tone la mwisho la maji hayo. Mpaka amalize kutawadha akiwa ametakasika kutokana na madhambi”. Muslim [244], Tirmidhiy [02], Ahmad [02/303], Ibn Maajah [283] & Nasaai [103]-Allah awarehemu.