HADITHI YA WIKI

 

Mtu mmoja alipo kuwa anatembea akazidiwa na kiu, akateremka kisimani, akanywa maji kisimani humo, kisha akatoka. Mara akamuona mbwa kinywa wazi, ulimi nje, anakula mchanga kutokana na kiu. Yule mtu akajisemea (moyoni mwake): Yamemfika (mbwa huyu) yale yaliyo nifika mimi. Yule mtu akajaza khufu (kiatu) yake maji akaiuma kwa kinywa chake, kisha akapanda kutoka kisimani. Akamnywesha yule mbwa, Allah akamsamehe (na kumuandikia tendo hilo jema). Wakauliza (Maswahaba): Ewe Mtume wa Allah! Hivi tunapata sisi ujira kwa kuwahudumia wanyama? Akajibu (Mtume): Katika kila ini bichi (kila kiumbe hai), kuna malipo (katika kukihudumia)”. Bukhaariy [03/551]

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *