“Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-alimbusu (mjukuu wake) Hassan bin Aliy na mbele yake alikuwepo Al-Aqra’a bin Haabis wa kabila la Tamim, amekaa. Akasema Al-Aqra’a: Hakika mimi nina watoto kumi, hakuna hata mmoja ninaye mbusu kati yao. Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-akamuangalia, kisha akasema: Asiye na huruma kwa wengine, hawezi kuhurumiwa”. Bukhaariy [08/26]